Date: 
20-09-2019
Reading: 
Psalm 15:1-5 (Zaburi 15:1-5)

FRIDAY  20TH SEPTEMBER 2019      MORNING                          

Psalm 15:1-5 New International Version (NIV)

1 Lord, who may dwell in your sacred tent?
    Who may live on your holy mountain?

2 The one whose walk is blameless,
    who does what is righteous,
    who speaks the truth from their heart;
3 whose tongue utters no slander,
    who does no wrong to a neighbor,
    and casts no slur on others;
4 who despises a vile person
    but honors those who fear the Lord;
who keeps an oath even when it hurts,
    and does not change their mind;
5 who lends money to the poor without interest;
    who does not accept a bribe against the innocent.

Whoever does these things
    will never be shaken.

This psalm reminds us that God is as interested in the way we treat others, as He is in our formal worship service.  In a true worship experience we relate to God both in spirit and life. True worship means to offer ourselves as “living sacrifices” expressed in a life of obedience to God. And such obedience reveals its true character in the way we relate to others. God expects not only the best formal worship service that we can offer to Him, but He also expects to be praised by the life we live outside the church building. Our daily lives have a deep meaning since they define the quality of the offering we bring to God.

The psalm invites us to acknowledge our limitations, inabilities, and failures. As we do so, we plead for God’s forgiveness and healing so that He will make us able to offer Him the kind of life and relationships he expects from us.


IJUMAA TAREHE  20 SEPTEMBA 2019       ASUBUHI                        

ZABURI 15:1-5

1 Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu?
Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake,
Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake.
Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu wamchao Bwana Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.
Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.

Zaburi hii inatukumbusha kuwa Mungu anatazama jinsi tunavyowatendea wengine kwa namna ile ile anavyozitazama ibada zetu za kila siku. Katika ibada ya kweli tunahusiana na Mungu kwa njia ya imani na maisha yetu. Ibada ya kweli maana yake ni kujitoa maisha yetu kuwa dhabihu iliyo hai inayoonekana kupitia maisha ya utii mbele za Mungu. Utii huo unadhihirishwa na jinsi tunavyohusiana na kuwatendea wengine. Mungu hatarajii tu kuona tunafanya ibada nzuri sana kanisani, lakini pia anatarajia kutukuzwa na yale maisha tunayoishi nje ya jengo la kanisa. Maisha yetu ya kila siku yana maana kubwa sana kiimani kwa sababu yanaeleza ubora au uzuri wa ile sadaka tunayoleta mbele za Mungu wetu.

Zaburi hii inatualika kutambua mapungufu yetu; na kwa kufanya hivyo, tunajiweka katika hali ya kuomba kusamehewa na Mungu na kuponywa madhaifu yetu ili atupe uwezo wa kuishi maisha yanayompendeza.