MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 11 JANUARI, 2026
SIKU YA BWANA YA 1 BAADA YA UFUNUO
NENO LINALOTUONGOZA NI
UBATIZO WETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 04/01/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 04/01/2026 ni Washarika 770 na Sunday School 193
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi/walezi kuwaandikisha watoto waliofika umri wa kuanza mafundisho ya Kipaimara. Atakaye hitaji kumuandikisha mtoto afike ofisi ya Parish Worker, Pia tarehe 17.01.2026 tunaanza mafundisho.
8. Leo tarehe 11/01/2026 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.
9. Uongozi wa Umoja wa wanawake unapenda kuwataarifu wasahrika kuwa wamevuna asali kutoka kwenye mizinga yao ya Tabora hivyo jumapili ijayo 18.01.2026 watauza asali mbichi katika ibada zote washarika mjiandae.
10. Washarika ambao bado hawajaza fomu za mwaka huu wachukue fomu kwa wazee wa Kanisa, vile vile fomu zitapatikana ofisini katikati ya wiki. Kwa washarika wapya wafike ofisini ili waweze kupewa utaratibu wa kupata bahasha.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: usharikani kwanzia saa moja
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
