Date:
11-12-2025
Reading:
2 Timotheo 3:10-13
Hii ni Advent
Alhamisi asubuhi tarehe 11.12.2025
2 Timotheo 3:10-13
10 Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,
11 na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.
13 lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
Changamkeni Mkombozi yu karibu;
Paulo baada ya kufundisha juu ya uovu wa siku za mwisho, anamtaka Timotheo kuuepuka huo uovu. Anamtaka kufuata mafundisho ya neno la Mungu akikaa katika imani na uvumilivu. Paulo anasisitiza upendo, saburi, kuvumilia mateso na maisha ya utauwa. Kuishika ile imani toka mwanzo ndiyo nguzo muhimu kama Paulo anavyoendelea kumuandikia Timotheo;
2 Timotheo 3:14-15
14 Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; 15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.Somo linaonesha Paulo akimsisitiza Timotheo kufundisha watu kuishika imani siku zote, ili Yesu akirudi awakute tayari. Ni wito wa kutengeneza maisha yetu, tayari kumlaki Bwana arudipo. Yesu anakuja, tujiandae kumpokea. Amina
Siku njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
