Jumamosi asubuhi tarehe 30.08.2025
Esta 4:12-17
12 Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta.
13 Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote.
14 Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?
15 Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,
16 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
17 Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.
Haki huinua Taifa;
Hamani alipanga kuwaangamiza Wayahudi wote katika ufalme wa Ahasuhero. Ikawa habari ya hofu kwa Wayahudi wote katika Ufalme huo. Katika somo la asubuhi ya leo Esta malkia anapelekewa ujumbe wa kutumia nafasi yake kujiokoa yeye na Wayahudi. Halikuwa jambo jepesi, lakini Esta alifanikiwa kuingia kwa Mfalme, Hamani aliuawa na Wayahudi wakapona kuangamizwa kama alivyokuwa ametoa taarifa Hamani.
Somo hili kwa asubuhi lina haya yafuatayo;
1. Hamani alikuwa katili, alimshawishi Mfalme kuwaangamiza Wayahudi kwa kuwaua. Hii haikuwa haki. Hamani ni mfano mbaya wa haki.
2. Esta alitumia nafasi yake vizuri mbele ya mfalme kuwaokoa Wayahudi wasiuawe. Tutumie nafasi zetu vizuri kuwapa watu haki zao.
3. Mfalme aliridhia Wayahudi wasiuawe, alitumia nafasi yake vizuri. Kama hapo juu no 2, tutumie nafasi zetu kwa haki
4. Hamani alipanga kuwaua Wayahudi lakini aliishia yeye kuuawa. Mshahara wa dhambi ni mauti. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650