Date:
03-03-2025
Reading:
Yohana 7:33-36
Jumatatu asubuhi tarehe 03.03.2025
Yohana 7:33-36
33 Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka.
34 Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja.
35 Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani?
36 Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?
Yesu anayaendea mateso Yerusalemu;
Yesu alikuwa anakaribia kuiendea njia ya mateso, hivyo alikuwa anawaambia wanafunzi wake mambo ambayo yangetokea. Anatumia lugha ya "kitambo kidogo nipo nanyi, kisha naenda zangu..." Mahali pengine katika Injili ya Yohana imeandikwa vizuri, kwamba kitambo kidogo hamnionii, kitambo kidogo mtaniona. Hapa alikuwa anaongelea kufa kwake na kupaa mbinguni;
Yohana 16:16-18
16 Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. 17 Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba? 18 Basi walisema, Neno gani hilo asemalo; hilo, Bado kitambo kidogo? Hatujui asemalo.Yesu alikuwa anaongelea juu ya kufa (hamnioni) na kufufuka (mtaniona) kwake katika kuukomboa ulimwengu. Inatukumbuka kukaa na Yesu aliyeteswa na kufa kwa ajili yetu, sasa na hata milele. Amina
Jumatatu njema
Heri Buberwa