MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 FEBRUARI, 2025 

SIKU YA BWANA YA 8 KABLA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA SIKU NI  

NENO LA MUNGU NI SILAHA IMARA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Mgeni aliyetufikia na cheti ni Twijisye-Santembe toka usharika wa Lukasi Dayosisi ya Konde. Amekuja kwenye matibabu. Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 16/02/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 16/02/2025 ilikuwa ni washarika 777. Sunday School 91. 

6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

7. Leo tarehe 23/02/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.

8. Jumapili ijayo tarehe 02/03/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

9. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=. 

10. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kuwa, kama kuna mtu anayo maoni yoyote juu ya usharika huu aandike maoni yake kwenye box la Maoni. Box letu la Maoni lipo karibu na kabati za namba zetu za bahasha.  

11. Tunapenda kuwatangazia washarika wote kuwa matayarisho ya igizo la Mateso ya Yesu yameanza. Mazoezi yatakuwepo kila Jumamosi saa 10:00 jioni katika ukumbi wa chini, wa Jengo la ofisi. Kwa tangazo hili tunawasihi washarika wa marika yote kushiriki katika kutayarisha igizo hili. Kwa Mawasiliano zaidi, wasiliana na Mwl. Lazaro Kibiwi, au Mzee Simon Jengo Mwenyekiti Misioni na Uinjilisti.

12. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha wanawake kwa matukio ya mwezi wa tatu.

13. Ijumaa tarehe 07/03/2025 ni siku ya maombi ya dunia yatafanyika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 3.00 asubuhi. Hivyo kwa wale ambao wataanzia hapa Kanisani safari itaanza saa moja kamili asubuhi

14. Jumapili tarehe 09/03/2025 siku ya Wanawake kuongoza ibada Sharika na Mitaa yote ngazi ya Dayosisi. Hivyo siku hiyo Wanawake wataongoza ibada zote.

15. Jumatano tarehe 12/03/2025 siku ya kurudia maombi katika ibada. Siku hiyo pia wanawake wataongoza ibada. 

16. SHUKRANI: JUMAPILI IJAYO TAREHE 02/03/2025 KATIKA IBADA YA KWANZA SAA 1.0O ASUBUHI

  • Familia ya Dr. na Bibi Albert Magohe watamshukuru Mungu kwa neema za Mungu juu ya familia yao, Mtoto wao Emani kutimiza mwaka mmoja na Mama pia kuongeza mwaka mwingine pamoja na kutimiza miaka 2 ya ndoa yao.

Neno: Warumi 8:28-30, Wimbo: TMW 149

17. NDOA:

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 01/03/2025. NDOA HII ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT DOVYA KATI YA

  • Bw. Goodluck Malimbwi Singano na Bi. Magreth Francis Mdoe  

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na Duka letu la Vitabu.

18. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
  • Upanga: Kwa Mama Frida Ndosi
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana Allen David
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Kimweri
  •  
  • Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.

19. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.org, pia tupo Facebook na Instagram.

 20. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili  

  Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.