Date: 
13-01-2025
Reading: 
Mathayo 3:13-17

Hii ni Epifania 

Jumatatu asubuhi tarehe 13.01.2025

Mathayo 3:13-17

13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.

14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?

15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.

16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Wabatizwao ni warithi wa uzima wa milele;

Sura ya 3 ya Injili ya Mathayo inahusika na Yohana Mbatizaji (mstari wa 1 hadi 12) akitangaza ujio wa Yesu Kristo. Anamtaja kama Mwokozi atakayekuja kuokoa Ulimwengu. Yohana aliwaita watu kutubu dhambi na kubatizwa, akisema Yesu ajaye angebatiza kwa Roho Mtakatifu tofauti na Yohana mwenyewe ambaye alibatiza kwa maji.

Baada ya mstari wa 12 ndipo somo la asubuhi ya leo linaanza, kwa kumuonesha Yesu akitaka kubatizwa na Yohana. Tunaona baada ya Yesu kubatizwa akitambulishwa na sauti kutoka mbinguni kama mwana mpendwa. 

Yesu anayetambulishwa kama mwana mpendwa, ndiye huyo kwa njia ya neno lake sisi tumebatizwa kwa ubatizo wenye nguvu ya Roho Mtakatifu kama alivyosema Yohana. Tunaalikwa kumsikia huyu Yesu Kristo, lakini zaidi kuuishi ubatizo wetu katika yeye ili atupe uzima wa milele. Amina

Uwe na wiki njema.

 

Heri Buberwa