Jumatano asubuhi 27.11.2024
Ufunuo wa Yohana 22:1-5
[1]Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,
[2]katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
[3]Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;
[4]nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.
[5]Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
Baada ya maisha haya, uzima wa milele
Yohana kabla ya kuhitimisha ufunuo wake, anaoneshwa mto wa maji ya uzima kutoka kiti cha enzi cha Mungu na Mwana-Kondoo. Anaoneshwa sehemu yenye raha kwa watakatifu wakakaouingia ufalme wa Mungu. Yohana anaoneshwa mbingu ambayo watakaoingia watamwona Bwana, wakitawala milele.
Wajibu wetu ni kutafakari, kwamba tumejiandaa vipi kuuingia mji huu ambao Yohana anaoneshwa. Tafakari kama mwenendo wako utakuingiza mbinguni. Amina
Uwe na Jumatano njema
Heri Buberwa