Jumamosi asubuhi tarehe 23.11.2024
Mathayo 13:24-30
24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo.
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Jiandae kwa hukumu ya mwisho;
Yesu anatoa mfano wa mwenye shamba aliyepanda mbegu njema, adui akaja kupanda magugu shambani. Watumwa walitaka kuyaondoa magugu shambani, mwenye shamba akawazuia. Akawaambia waviache vyote vikue pamoja hata wakati wa mavuno, ambapo mwishoni magugu yatachomwa, lakini ngano itakusanywa ghalani.
Mungu anatupa nafasi ya kutubu na kumrudia, kwa njia ya kutubu dhambi zetu. Anatupa rehema tunapotubu ili tumrudie. Maisha ya imani ya kweli, toba na msamaha ni muhimu ili kuurithi uzima wa milele. Tumia nafasi uliyopewa na Bwana kuhakikisha kuwa kabla hujalala umesamehewa dhambi zako. Amina
Siku njema
Heri Buberwa