Date: 
12-07-2024
Reading: 
Mhubiri 10:18

Ijumaa asubuhi tarehe 12.07.2024

Mhubiri 10:18

Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.

Bidii ya kijana, mafanikio ya Kanisa;

Nyumba isiyojengwa kwa vigezo stahiki huwa siyo imara, kama ambavyo mwandishi wa somo anaandika. Nyumba hiyo huwa mbovu sehemu kadhaa kulingana na ujenzi wake. Kumbe nyumba inapojengwa ni muhimu na lazima kuweka mazingira na mahitaji muhimu kuanzia eneo la ujenzi, fundi na vifaa, bila kusahau usimamizi madhubuti ili nyumba iwe nzuri na imara.

Lugha ya 'nyumba mbovu' imetumika kueleza jinsi ambavyo uvivu unaweza kufanya tusifanikiwe. Ujenzi mbovu huleta nyumba mbovu. Vile vile kukosa umakini katika kazi, uvivu, kutowajibika na kutojali huleta mafanikio hafifu. Uvivu ni dhambi, tuache mara moja. Amina

Heri Buberwa