Date: 
24-05-2024
Reading: 
1Wakorintho 12:1-3

Ijumaa asubuhi tarehe 24.05.2024

1 Wakorintho 12:1-3

1 Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu.

2 Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.

3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu kwa kila aaminiye;

Mtume Paulo anawakumbusha watu wa Kanisa la Korintho maisha yao ya zamani ambapo hawakumuamini Kristo. Waliishi pasipo kumjua Kristo, kwa maana hiyo hawakumuamini Mungu wa kweli. Sasa anawaambia kuwa kwa kumpokea Yesu Kristo, wanaye Roho Mtakatifu aliye mpatanishi na Mungu kweli.

Mtume Paulo anatukumbusha kuacha maisha ya zamani na kuishi kama Kristo anavyotaka baada ya kumpokea yeye. Tunaacha maisha ya zamani tunapoongozwa na Kristo mwenyewe kwa njia ya neno lake. Tukiwa na Kristo, Roho Mtakatifu anakuwa ndani yetu daima. Hapo ndipo tunaweza kupata msaada wa daima kuelekea uzima wa milele. Amina.

Ijumaa njema

Heri Buberwa