Date: 
02-11-2023
Reading: 
2 Mambo ya nyakati 34:29-33

Alhamisi asubuhi tarehe 02.11.2023

2 Mambo ya Nyakati 34:29-33

29 Ndipo mfalme akapeleka wajumbe, akawakusanya wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.

30 Akapanda mfalme nyumbani kwa Bwana, na watu wote wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, na makuhani na Walawi, na watu wote, wakubwa kwa wadogo; naye akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana nyumbani mwa Bwana.

31 Akasimama mfalme mahali pake, akafanya agano mbele za Bwana, kumfuata Bwana, na kuzishika amri zake, na shuhuda zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, kuyatenda maneno ya agano yaliyoandikwa kitabuni humo.

32 Akawafanya wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini walikubali. Na wenyeji wa Yerusalemu wakafanya sawasawa na agano la Mungu, Mungu wa baba zao.

33 Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie Bwana, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata Bwana, Mungu wa baba zao.

Tutengeneze mambo yaliyoharibika;

Yosia mwana wa Daudi alianza kutawala akiwa na miaka minane, akaanza kuutafuta uso wa Mungu wa babaye. Alipofikisha miaka minane akaondoa sanamu na alama zote mahali pote pa utawala wake. Akaamuru nyumba ya Bwana kusafishwa. Katika kusafisha hekalu, wale waliotumwa kusafisha nyumba ya Bwana wakapewa kitabu na Kuhani kilichokuwa na ujumbe wa Bwana.

Ujumbe uliokuwa kwenye kitabu huu hapa;

2 Mambo ya Nyakati 34:23-25

23 Akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mwambieni mtu huyo aliyewatuma kwangu,
24 Bwana asema hivi, Angalia, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, na juu ya wakaao, laana zote zilizoandikwa katika kitabu hicho walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda;
25 kwa sababu wameniacha mimi, na kuifukizia uvumba miungu mingine, ili wanikasirishe mimi kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo ghadhabu yangu imemwagika juu ya mahali hapa, wala isizimike.

Ndipo sasa tunasoma Mfalme akipanda nyumbani mwa Bwana, na watu wake. Ujumbe wa kitabu kile unasomwa. Ujumbe unapokelewa, Mfalme na watu wake wanaweka ahadi ya kumtumikia Bwana na kushika amri zake.

Sisi tunalo Agano na Bwana, kumwamini na kumtumikia hata kufa, kama tulivyokiri siku ya Kipaimara. Israeli walitengeneza mambo yaliyoharibika, wakaahidi kumcha Bwana. Nasi tutengeneze palipoharibika, ili tukae na Kristo, leo na siku zote. Amina.

Heri Buberwa