Date: 
09-02-2022
Reading: 
Mathayo 17:1-8

Jumatano asubuhi tarehe 09.02.2021

Mathayo 17:1-8

1 Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani;

2 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.

3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.

4 Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.

5 Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.

6 Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.

7 Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope.

8 Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake.

Utukufu wa Mwana wa Mungu;

Yesu aling'aa mbele ya Petro, Yakobo na Yohana. Aligeuka sura mavazi yake yakawa meupe. Pale akatokea Elia na Musa. Ukisoma mstari wa 9, Yesu anawatuma akina Petro kutomwambia yeyote yaliyotokea, hadi atakapofufuka;

Mathayo 17:9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.

Kwa nini hadi afufuke?

Kung'aa lilikuwa jambo la muda tu, lakini ufufuko ulikuwa ni kwa ajili ya uzima wa milele. Yesu aligeuka sura kama alama ya upatanisho kati ya wanadamu na Mungu, na baadae akafa na kufufuka. Mwisho alipaa mbinguni kwa utukufu wake, ambapo atarudi kulichukua Kanisa. Uko tayari kuingia mbinguni? Basi, anakuita kumpokea katika Utukufu wake.

Siku njema.