MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 30 OKTOBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MATENGENEZO YA KANISA, USHUHUDA WETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 23/10/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. AlhamisiMaombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa Pili yatafanyika tarehe 19/11/2022 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana hapa Usharikani. Wale waliopata Kipaimara wenye umri wa miaka 15 pia wanakaribishwa kwenye mafundisho haya. Wazazi na Walezi mnaombwa kuandikisha watoto watakaohudhuria kwa Parish Worker ili kufanya maandalizi haya.

6. SHUKRANI

Jumapili ijayo tarehe 6/11/2022 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi familia ya Bibi Violet Maro watamshukuru Mungu kwa maisha ya Baba yao Dr. Fanuel Maro aliyetwaliwa na Bwana miaka kumi iliyopita pamoja na Neema, fadhili kwa familia yao.

Neno: Zaburi 117, 

7. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 05/11/2022  

SAA 6.00 MCHANA

Bw. Victor Frank Koyanga na Bi. Annansia Godbless Uronu

Matangazo mengine yapo kwenye ubao wa Matangazo.

8.  NYUMBA KWA NYUMBA 

Masaki na Oyserbay: kwa Bwana na Bibi Aaron Ndasiwa

 

Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa …

  • Kinondoni: Kwa Dr. na Bibi Onesmo
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Tom Njau

9. Zamu: Zamu za wazee ni Wazee wote.