MATANGAZO YA USHARIKA,  TAREHE 22 JANUARI, 2023                     

NENO LINALOTUONGOZA NI: YESU ANAONDOA UBAGUZI                     

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 15/01/2023

    Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wakumtolea kwa hiari mali            alizotupa kwa kazi yake.

    NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

    0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

     Namba ya Wakala M-PESA 5795794KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa  Uongozi wa Mungu, Ibada za  mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu.  Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Kwaya ya Agape/walezi wa kwaya watatembelea wahitaji katika hospital ya Muhimbili, wakilenga zaidi kuwafikia watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wapatao 100 kwa kuwachangia bima ya afya kwa kila mtoto gharama yake ni sh @50,400/= pamoja na vitu kama sabuni, mafuta ya kupata,miswaki,nguo size mbali mbali,juice,maji nk, Wanaomba washarika muwaunge mkono kwenye huduma hii, Ofisi ya Parish weka na mhasibu itapokea sadaka hii Mungu awabariki!

6. Jumapili ijayo tarehe 29/01/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana.  Washarika tujiandae.

7. Jumamosi ijayo tarehe 28/01/2023 Jumuiya ya mjini kati watafanya ibada hapa Usharikani ikiambatana  na kutoa shukrani yao.  Washarika wote wa mjini kati mnaombwa kuhudhuria. Pia kuna wengine wanaishi maeneo ya mjini kati lakini hawakufahamu wapi waende sasa wafike jumamosi ili waweze kuungana  jumuiya yao vizuri.

8. SHUKRANI

Jumapili ijayo tarehe 29/01/2023 katika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi Catherine Mushi  pamoja na familia atamshukuru Mungu kwa Mambo mengi ambayo amemtendea.

Neno:  Zaburi 28:7, Wimbo: TMW 295

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana Dudley Mawalla
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Watatangaziana           
  • Mjini kati: Kwa hapa Usharikani
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Rweikiza
  • Kinondoni: Kwa Prof.  G. Mmari                                       
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Kevela 
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mbwilo
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Watatangaziana   
  • Tababa:Watatangaziana   

10. NDOA.

Hakuna Ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

11. Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu,  Bwana ayabariki.