MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 16 JANUARI, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MUNGU HUTAKASA NYUMBA ZETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. 

3. Matoleo ya Tarehe 09/01/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu pamoja na Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.30 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Wazazi na Walezi wenye watoto wanaoanza Kipaimara mwaka wa Kwanza 2022 wafike Ofisi ya Parish Worker ili wajiandikishe. Umri ni kuanzia miaka 12 na kuendelea.

6. Tunamshukuru Mungu kwa kumaliza Semina ya maombi ya kufungua Mwaka ya wiki mbili, iliyomalizika Ijumaa tarehe 14/01/2022 kwa kishindo, kwani Mungu wetu ameadhimishwa. Tunawapongeza wote walioweza kushiriki na tunawaombea lile agano walilopatana na Mungu liwe ushuhuda kwao, na kwa Mungu wetu. Aidha tutaendelea na Maombi na Maombezi siku ya Alhamisi tarehe 20/01/2022 saa 11.30 jioni. Wote mnakaribishwa.

7. Shukrani:

Jumapili ijayo tarehe 23/01/2022 katika ibada ya kwanza familia ya Mama Violet Japhet Minja watamshukuru Mungu kwa kuwawezesha kumaliza salama msiba wa mama yao mpendwa uliotokea huko Rombo, Moshi tarehe 13/11/2021 pamoja na kuwakirimia baraka nyingi mno maishani mwao.

Neno: Zaburi 23.

8. NDOA.

Matangazo ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

9. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.