MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 06 JANUARI, 2019

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

TUMEITWA KUFANYA KAZI YA MISIONI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Mgeni aliyefika na cheti ni:-  Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

 

3. Alhamisi ijayo tarehe 10/01/2019 saa 11.30 jioni hapa usharikani tutakuwa na kipindi cha  maombi na maombezi, mnenaji atakuwa   Mwinjilisti Baraka Mbise kutoka KKKT Usharika wa Ubungo.  Wote mnakumbushwa kuliombea kusanyiko hilo na kuhudhuria.

4. Nyumba kwa nyumba

Ni jambo la kumshukuru Mungu, katika sura ya Yesu Kristo, kwamba tumepata kibali kuingia mwaka 2019.  Uongozi wa Usharika unapenda kuwakaribisha tena na kuwahamasisha kuanza kwa ari na nguvu zote kuabudu pamoja kupitia vikundi vyetu vya ibada, au jumuiya kwa kuutafuta uso wa Mungu na kujengana ki-imani.  Ingependeza sana na kujenga uimara wa jamii zetu kama kila kaya na familia  ya Washarika wa Kanisa Kuu Azania Front atakuwa amejiunga na Jumuiya mojawao kati ya zilizopo sasa, na kama kuna umbali unaokuzuia kuungana na wenzio tafadhali wasiliana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwakili; Mzee Theophilus Mlaki, au Mwenyekiti wa Misioni na Uinjilisti Mzee Simon Jengo kwa ushauri na msaada.  Tufanye bidii za kutafuta na kujiunga na jumuiya zetu.  Mungu awabariki sana kwa utayari wenu.  Kitabu cha Mwongozo wa masomo ya ibada za nyumba kwa nyumba kilichotayarishwa na uongozi wa Dayosisi yetu, kimetoka na kinapatikana katika Duka letu la vitabu kwa bei ya sh. 2000 tu.

5. Washarika mnaendelea kukumbushwa kujaza fomu na kuzipitisha kwa viongozi wenu wa jumuiya ili waziwasilishe Ofisini. Hii ni kwa ajili ya kuwa na kumbukumbu sahihi kwa mwaka 2019,Namba za bahasha za Ahadi ni zile mpyazilizotolewa mwaka huu. Msharika ambaye atakuwa ajajaza fomu hii atahesabika kuwa hayupo na namba itafutwa na kupewa mtu mwingine

 

6. Shukrani:

Jumapili ijayo tarehe 13/01/2018 katika ibada ya kwanza Familia ya Bwana na Bibi Andrew Kuzilwa watamshukuru Mungu kwa mambo mema aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kufikisha miaka 15 ya Ndoa na kumwezesha Dada Martha Kuzilwa kupata ajira.

Neno: Zaburi. 95:1-7, Wimbo: 255 na Kwaya ya Agape (Natembea)

Pia Jumuiya ya kikundi cha ibada cha Mwenge, Kijitonyama, Makumbusho, Sinza, Ubung na Makongo watatoa Sadaka ya shukrai madhabahuni kwa Bwana wakimshukuru Mungu kwa Ulinzi wake na kupata kibali cha kumwabudu na kutumika kwa mwaka mwingine tena.  Washarika wote wanakaibishwa kuwaombea na kuwasindikiza.

7. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Wazo/Tegeta/Kunduchi/Bahari Beach/Ununio: kwa Mchungaji Chuwa

- Mwenge,Kijitonyama, Makumbusho, Sinza, Ubungo na Makongo: Kwa Bwana na Bibi Simon Jengo.

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.