MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 08 APRILI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU KRISTO AJIFUNUA KWETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Mgeni aliyetufikia na cheti ni Elibariki Sabaya Mollel toka Usharika wa Ilboru Arusha, amekuja kikazi. lakini kama kuna wageni walioshiriki nasi mara ya kwanza wasimame ili tuweze kuwakaribisha.

3. Jumamosi ijayo ya tarehe 14/04/2018 saa 2.00 asubuhi hadi saa 3.30 asubuhi Jumuiya zote za Kanisa Kuu Azania Front zitakuwa na ibada ya pamoja hapa Usharikani.  Jumuiya zote zifike kwa ajili ya ibada hii.

4. Harambee ya Kiharaka itafanyika tarehe 06/05/2018. Ibada zitakuwa ni mbili na ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi siku hiyo.  Tunategemea kukusanya kiasi cha Tshs Milioni mia tatu (3,000,000/=) kwa kazi zote za umeme katika awamu hii ya ujenzi.  Ibada zote zitaongozwa na Baba Askofu Dr. Alex G. Malasusa.  Washarika tuiombee siku hiyo na kujiandaa kuifanikisha.

5. Jumapili ijayo tarehe 15/04/2018 katika ibada ya pili familia ya Prof. William Matuja watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kumaliza salama msiba wa Mke wake mpendwa Mzee wa Kanisa Esther Matuja  na kuendelea kuwafariji.

Neno: 1 Wathesalonike 5:18, Zaburi 138:1-3  Wimbo: TMW 175 na Kwaya Kuu (Yesu Mwokozi yu Mlinzi wangu)

6. Uongozi wa Kwaya ya Wanawake unapenda kuwatangazia wanawake wote kuwa Mazoezi ya nyimbo za Tamasha la Wanawake yameshaanza. Hivyo wanaomba wanawake wote wa Kwaya zote na wasio wanakwaya waungane kwa pamoja kwenye mazoezi ya maandalizi ya Tamasha.  Mazoezi ni kila siku ya Jumatano na Ijumaa kuanzia saa 10.00 jioni.  Mnakaribishwa sana.

7. Uongozi wa Umoja wa Wanawake Azania unapenda kutoa taarifa kuwa kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka jumamosi ijayo tarehe 14/04/2018 saa 4.00 asubuhi.  Wanawake wote wanaombwa kuhudhuria ili kujua taarifa ya maendeleo na taarifa ya fedha ya umoja wa Wanawake.  Pia Uongozi wa Usharika Azania Front unapenda kuwatangazia wanawake wote kuwa Jumampili ijayo tarehe 15/04/2018 ni siku ya Uchaguzi wa Sharika na Mitaa yote.  Hivyo Wanawake wote wanaombwa kuhudhuria Uchaguzi wa Wanawake hapa Azania, uchaguzi huu utafanyika mara baada ya ibada ya Kwanza.  Kwahiyo Wanawake wa Kwaya KUu, Kwaya ya Vijana na Wanawake wote wanaosali ibada ya pili mnaombwa kuwahi kufika ili kufanya Uchaguzi huu.

 

NDOA.

KWA MARA YA TATU TUNANGAZA NDOA ZA TAREHE 14/04/2018. 

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Allen J. Mamkwe   na     Bi. Happy E. Temu

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

8. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

Upanga: Kwa Kizigha

Kinondoni: Watashiriki ibada ya pamoja  hapa Usharikani

Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watashiriki ibada ya pamoja  hapa Usharikani

Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Prof. Esther Mwaikambo

Mjini kati:  Watashiriki ibada ya pamoja  hapa Usharikani

Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Watashiriki ibada ya pamoja  hapa Usharikani

Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Watashiriki ibada ya pamoja  hapa Usharikani

Tabata:  Watashiriki ibada ya pamoja  hapa Usharikani

                                               

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.