MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 10 SEPTEMBA, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI JIRANI WETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti.

3. Kamati ya Misioni na Unjilisti inapenda kuwatangazia kwamba leo hakutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi bali kutakuwa na faragha ya maombi. Wote ambao wana msukumo wa kuomba tukutane saa kumi katika ukumbi wa chini kwa maombi. Ajenda za maombi ni kuombea washarika, Usharika wetu na mipango  ya Usharika iliyo mbele yetu, Dayosisi na Taifa.  Hiki sio kipindi cha maombezi bali ni maombi, usije ukitegemea kuombewa uje ukitegemea kuomba. Aidha  kipindi cha maombi na maombezi kitakuwa siku ya alhamisi tarehe 14.09.2017 saa 11.00 jioni na kitaongozwa na Mwinjilisti Emmanuel Frank wa KKKT Tumbi.  Kwa kujitayarisha kwa kipindi hiki cha Alhamisi wote tusome kitabu cha Joshua sura ya 5 na 6. Hii ni nafasi ya pekee ya kumkaribia Mungu na haja zetu. Wote mnakaribishwa.

4. Vitenge vya Miaka mia tano ya matengenezo ya Kanisa vipo.  Vitauzwa kuanzia siku ya Jumanne hapa Usharikani kwa bei ya sh. 15,000/=.  Hivyo atakayehitaji apeleke fedha kwa Parish Worker au viongozi wa Umoja wa Wanawake.  Aidha Vitenge vya Kiharaka bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10.  Kama umeshanunua unaweza kumnunulia ndugu, rafiki ili tuweze kufanikisha ujenzi wa kituo chetu cha Kiroho Kiharaka.  

5. Ijumaa ijayo tarehe 15/09/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha kamati ya utendaji ya Baraza la wazee.

6. Kamati ya Afya na Ustawi wa Jamii Azania Front inapenda kuwataarifu kuhusu mabadiliko ya tarehe ya Semina ya Elimu ya Afya kwa watoto wa Kipaimara 2017.  Kutokana na sababu zisizozuilika semina hii sasa itafanyika tarehe 16/09/2017 badala ya tarehe ya awali 23/09/2017.  Aidha kutokana na mabadiliko hayo Semina ya mwaka huu itawahusu watoto wa Kipaimara tu na wale waliohitimu hivi karibuni wenye umri hadi miaka 15.  Semina iliyatarajiwa kufanyiwa wazazi wa watoto hawa itafanyika mwakani.  Tunaomba samahani kwa usumbufu uliojitokeza na tuiombee sana siku hiyo.

7. Jumapili ijayo tarehe 17/09/2017 tutashiriki Chakula cha Bwana. Hivyo kama kawaida ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika tujiandae. Aidha kama kuna mgonjwa nyumbani anahitaji huduma ya Chakula cha Bwana mnaombwa kutoa taarifa ofisini kwa Mchungaji.

8. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwaarifu wazazi wote kuwa, mwaka huu watoto watavaa Tshirt za miaka miatano ya matengenezo ya Kanisa katika sikukuu yao ya Mikaeli na Watoto.  Hivyo tunaomba wazazi muwanunulie watoto Tshirt hizo.  Bei ya TShirt  moja ni sh. 10,000/=.  Wazazi mnaombwa kupeleka fedha hizo kwa mhasibu wa Usharika ili zikachukuliwe kwa pamoja.

9. Jumapili ijayo tarehe 17/09/2017 katika ibada ya saa 1.00 asubuhi familia ya Mzee Elinaja Lyimo itamshukuru Mungu  kwa ajili ya kuwapa nguvu wakati wa msiba wa baba yao Mzee Elinaja Abel Lyimo  na namna anavyoendelea kuwapigania hata sasa.

Neno: Zaburi 23,  Wimbo: TM 262 na 135.

 

10. Jumanne ijayo tarehe 12.09.2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na maombi ya viongozi wa nyumba kwa nyumba. Viongozi wote wanaombwa kuhudhuria na kwa wakati.

 

11. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 30/09/2017

NDOA HII ITAFUNGA  KANISA LA ANGLIKAN NEEMA CATHEDRAL RUBUNGO

Bw. Jossam Mugisha Mabaraza          na    Bi. Magreth Ernest Mtui

 

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 23/09/2017

NDOA HII ITAFUNGA  KANISA LA KATOLIKI ST. PETER

Bw. Paul Kennedy Ongoma      na    Bi. Shanga Prize Naomi Jackson Kaale

 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

 

12. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

 

  • Upanga: Kwa Mama Mbaga
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Edward Mkony
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Bwana na Bibi James Monyo
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Dr. na Bibi Kumbwaeli Salewi
  • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
  • Tabata: Watatangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Makwe
  • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Mally
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Dr. na Bibi Kashililah

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.