Date: 
06-12-2016
Reading: 
Isaiah 62:1-5 (NIV), Tues 6th Dec

TUESDAY 6TH DECEMBER 2016 MORNING                        

Isaiah 62:1-5 New International Version (NIV)

Zion’s New Name

1 For Zion’s sake I will not keep silent,
    for Jerusalem’s sake I will not remain quiet,
till her vindication shines out like the dawn,

    her salvation like a blazing torch.
The nations will see your vindication,
    and all kings your glory;
you will be called by a new name

    that the mouth of the Lord will bestow.
You will be a crown of splendor in the Lord’s hand,
    a royal diadem in the hand of your God.
No longer will they call you Deserted,
    or name your land Desolate.
But you will be called Hephzibah,
[a]
    and your land Beulah[b];
for the Lord will take delight in you,

    and your land will be married.
As a young man marries a young woman,
    so will your Builder marry you;
as a bridegroom rejoices over his bride,

    so will your God rejoice over you.

Footnotes:

  1. Isaiah 62:4 Hephzibah means my delight is in her.
  2. Isaiah 62:4 Beulah means married.

Isaiah brings words of encouragement from God to the Jews who are in captivity in Babylon. God tells them that He can not forget His people. God loves His people as a husband loves his bride.  God will restore His people.

Let these words be an encouragement to you too. If you are a true Christian part of the church of Christ you are precious to God too.    

 

JUMANNE TAREHE 6 DISEMBA 2016  ASUBUHI              

ISAYA  62:1-5

1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 
2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. 
3 Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 
4 Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako itaolewa. 
5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 
   

Maneno ya Nabii Isaya ni ujumbe wa Mungu kwa Taifa takatifu, watu wa Yuda. Ni maneno kuwatia moyo wakati walikuwa Utumwani kule Babeli. Mungu anawambia kwamba atawarudisha tena katika nafasi yao. Mungu anawapenda kama Bwana arusi anavyompenda bibi harusi.

Sisi Wakristo pia tunapendwa na Mungu. Sisi Kanisa, ni Bibi harusi wa Yesu Kristo na anatupenda. Maneno haya yawe faraja kwako, Mungu anakupenda.