Date: 
04-06-2019
Reading: 
Isaiah 38:1-8

TUESDAY 4TH JUNE 2019 MORNING                                        

Isaiah 38:1-8 New International Version (NIV)

Hezekiah’s Illness

1 In those days Hezekiah became ill and was at the point of death. The prophet Isaiah son of Amoz went to him and said, “This is what the Lord says: Put your house in order, because you are going to die; you will not recover.”

Hezekiah turned his face to the wall and prayed to the Lord,“Remember, Lord, how I have walked before you faithfully and with wholehearted devotion and have done what is good in your eyes.” And Hezekiah wept bitterly.

Then the word of the Lord came to Isaiah: “Go and tell Hezekiah, ‘This is what the Lord, the God of your father David, says: I have heard your prayer and seen your tears; I will add fifteen years to your life. And I will deliver you and this city from the hand of the king of Assyria. I will defend this city.

“‘This is the Lord’s sign to you that the Lord will do what he has promised: I will make the shadow cast by the sun go back the ten steps it has gone down on the stairway of Ahaz.’” So the sunlight went back the ten steps it had gone down.

Hezekiah prayed to God when he received God’s message through the prophet Isaiah. He asked for mercy from God to spare his life and reminded God that he had obeyed Him his life. God heard and answered King Hezekiah’s prayer and added another 15 years to his life. God also promised to rescue the city from the enemies.

Let us bring our requests to God in faith. God is willing to hear and answer our prayers.  He does not always answer our prayers as we wish but let us not give up praying.

JUMANNE TAREHE 4 JUNI 2019 ASUBUHI                                        

ISAYA 38:1-8

1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. 
Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana, 
akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. 
Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, 
Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano. 
Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu. 
Jambo hili liwe ishara kwako, itokayo kwa Bwana, ya kuwa Bwana atalitimiza jambo hili alilolisema; 
Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka. 
 

Nabii Isaya alileta ujumbe kutoka Mungu kwa Mfalme Hezekia. Alisema kwamba Hezekia atakufa. Hezekia hakutaka kupokea ujumbe huu. Alimlilia Mungu katika maombi na alimkumbusha Mungu jinsi alivyokuwa mtiifu kwake. Mungu alisikia maombi yake na alimjibu. Mungu alimwongezea Mfalme  Hezekia miaka 15 ya kuishi, pia aliahidi kulinda mji wake dhidhi ya adui.

Tulete mahitaji yetu mbele ya Mungu tukiomba kwa imani. Mungu anasikia na anajibu maombi. Si kila wakati anajibu kama tunavyotaka lakini tusikate tamaa. Tuendelee kuomba.