Date: 
06-12-2018
Reading: 
Isaiah 19:19-22 (Isaya 19:19-22)

THURSDAY  6TH DECEMBER 2018 MORNING                                

Isaiah 19:19-22 New International Version (NIV)

19 In that day there will be an altar to the Lord in the heart of Egypt, and a monument to the Lord at its border. 20 It will be a sign and witness to the Lord Almighty in the land of Egypt. When they cry out to the Lord because of their oppressors, he will send them a savior and defender, and he will rescue them. 21 So the Lord will make himself known to the Egyptians, and in that day they will acknowledge the Lord. They will worship with sacrifices and grain offerings; they will make vows to the Lord and keep them. 22 The Lord will strike Egypt with a plague; he will strike them and heal them. They will turn to the Lord, and he will respond to their pleas and heal them.

This is a prophecy that the Egyptians will come to faith in the true God.  There are some Christians in Egypt today but the church is not very strong. However early in church History the Egyptian church was very strong. Now the church is much stronger in Sub-Saharan Africa.  

God desires all people everywhere to come to faith in Him. Pray that God would raise up true churches all around the world and that the Gospel would be preached faithfully and many people would trust in Jesus Christ as their Lord and Saviour.     

ALHAMISI TAREHE 6 DISEMBA 2018 ASUBUHI                             

ISAYA 19:19-22

19 Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa Bwana, na nguzo mpakani mwake kwa Bwana. 
20 Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa Bwana wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia Bwana kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa. 
21 Na Bwana atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua Bwana katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea Bwana nadhiri, na kuzitekeleza. 
22 Naye Bwana atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa Bwana, atakubali maombi yao na kuwaponya. 

Isaya anatabiri Watu wa Misri watamwabudu Mungu wa kweli . Kuna Kanisa lipo Misri lakini halina nguvu sana. Injili ilifika Misri mapema kwa sababu ni karibu na Israeli. Kanisa la Misri ilikuwa na nguvu zamani kabala Uisalamu kuingia.

Injili ilifika Tanzania na nchi zingine kusini mwa Sahara baadaye sana, lakini kanisa ilipata nguvu katika nchi nyingi. 

Mungu anatamani watu wote wafikiwe na Injili na kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wao. Tuombee Injili ihubiriwe duniani kote.