Date: 
31-03-2017
Reading: 
Deuteronomy 8:6-10 (NIV)

SATURDAY 1ST APRIL 2017 MORNING                          

Deuteronomy 8:6-10 New International Version (NIV)

Observe the commands of the Lord your God, walking in obedience to him and revering him. For the Lord your God is bringing you into a good land—a land with brooks, streams, and deep springs gushing out into the valleys and hills; a land with wheat and barley, vines and fig trees, pomegranates, olive oil and honey; a land where bread will not be scarce and you will lack nothing; a land where the rocks are iron and you can dig copper out of the hills.

10 When you have eaten and are satisfied, praise the Lord your God for the good land he has given you.

God promised His people the Israelites that He would give them a good land. The land would be fertile and produce a good harvest and the people would eat and be satisfied.

God reminds them to obey His commands and walk in His ways and to be thankful for all He has given them.

Let us obey God all our lives and be thankful to Him for all His blessings to us.

JUMAMOSI TAREHE 1 APRILI 2017 ASUBUHI        

KUMBUKUMBU LA TORATI 8:6-10

6 Nawe uzishike amri za Bwana, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha. 
7 Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima; 
8 nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali; 
9 nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba. 
10 Nawe utakula ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. 
 

Mungu aliwapa Waisraeli nchi nzuri yenye rutuba. Nchi itakayozaa matunda na mazao mazuri. Watakula na kushiba. Mungu anawasihi wawe watu wa shukrani pia watii amri zake na watembee katika njia za Mungu.

Sisi pia tunapaswa kumtii Mungu na kufanya mapenzi yake katika maisha yetu na tuwe watu wa shukrani.