Date:
28-12-2024
Reading:
Mathayo 10:16-19?
Hii ni Noeli
Jumamosi asubuhi tarehe 28.12.2024
Mathayo 10:16-19
[16]Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
[17]Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
[18]nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
[19]Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
Uwe shahidi mwaminifu wa Kristo hata kufa;
Yesu alikuwa akiwatuma kazi wanafunzi wake, akiwaambia kuwa kazi ya utume siyo rahisi. Ni kazi ngumu yenye kukataliwa mahali pengine. Katika mstari wa 19 anawapa njia sahihi, kuwa wamtegemee yeye katika kazi hiyo.
Siyo rahisi maisha yetu kuendelea kuwa yenye ushuhuda wa Kristo, na kwa nguvu yetu hatuwezi kudumu tukiwa mashahidi waaminifu bila msaada wa Mungu. Ni kwa neema yake tunaweza yote, hivyo hatuna budi kudumu katika Imani ya kweli na sala ili tutimize wajibu tuliopewa. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa