Date:
12-12-2024
Reading:
Zaburi 108:10-13
Hii ni Advent
Alhamisi asubuhi tarehe 12.12.2024
Zaburi 108:10-13
[10]Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma?
Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?
[11]Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?
Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?
[12]Utuletee msaada juu ya mtesi,
Maana wokovu wa binadamu haufai.
[13]Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,
Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.
Ukombozi wetu umekaribia;
Daudi anamuita Bwana asimuache katika njia zake. Daudi anakiri kuwa wokovu wa mwanadamu haufai, bali msaada wa Mungu ndio utoshao kwa mwanadamu kutenda yote.
Daudi anatukumbusha kumuita na kumtegemea Bwana katika njia yetu ya ufuasi. Hatuwezi kushinda kwa nguvu zetu, bali kwa msaada wa Mungu, tukiungojea ufalme wake.
Alhamisi njema.
Heri Buberwa
Mlutheri