Date:
28-09-2024
Reading:
Kumbukumbu la Torati 30:19-20
Jumamosi asubuhi tarehe 28.09.2024
Kumbukumbu la Torati 30:19-20
19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
20 kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
Uchaguzi wako ndiyo maisha yako;
Sura nzima ya thelathini imejaa laana na baraka. Laana ni pale ambapo Israeli wasingemwamini Bwana, na baraka ni pale ambapo wangekataa kumwamini Bwana. Mistari tuliyosoma ni hitimisho la sura ya thelathini, kukiwa na ahadi ya uzima na mauti, baraka na laana katika kumwamini Bwana.
Israeli wanaambiwa kuchagua uzima ili wawe hai wote na vizazi vyao.
Kama tulivyoona jana asubuhi, sisi wokovu wetu hauna masharti maana hatuko chini ya sheria. Hakuna habari ya uzima na mauti, wala baraka na laana. Ni habari njema kwamba tumeokolewa kwa neema, na wajibu wetu ni kumwamini Yesu ili tuwe na uzima tele, siku zote za maisha yetu. Mwamini sasa uokolewe. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa