DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI  

MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 28 JUNI, 2026 

SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA NI:

“TUMEITWA KUTENDA HAKI NA HURUMA”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti: 

3. Matoleo ya Tarehe 14/06/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 21/06/2026 ni Washarika 789 na Sunday School 240 

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4 :30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=. 

7. Uongozi wa Kwaya ya Umoja unaendelea kuwahimiza waimbaji wote kufika kwenye mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya reformation, mazoezi ni siku ya jumanne saa 11.00 jioni. Wanakwaya mnaombwa kufika kwa wingi na kwa wakati.

8. Jumapili ijayo tarehe 05/07/2026 katika ibada 3 saa 4.30 asubuhi familia ya Bwana na Bibi George Mnyitafu watamshukuru Mungu kwa Watoto wao Israel na Rehema Mnyitafu kufunga ndoa Takatifu.

Neno: Zaburi 28:7-8, Wimbo: Neema ya ajabu ametushushia (Kwaya Kuu) 

9. NDOA. Ndoa za washarika

 KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 11/07/2026

 SAA 7.00 MCHANA

 Bw. Erick godfrey Kimaro na Bi. Liben Geuken Mmary

 SAA 9.00 ALASIRI

 BW. Christopher Kelvin Chambo na Bi. Gillian Hope Mlowe

 Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Hapa Usharikani jumamosi saa moja asubuhi

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Moses Kombe

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Mama Elipendo Mkandawile

- Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Luty Makani

- Upanga: Kwa: Bwana na Bibi Happines Nkya

11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azaniafront.org, pia tupo Facebook na Instagram.

12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.