DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 21 JUNI, 2026
SIKU YA BWANA YA 3 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI:
“PAMOJA TUJENGE KANISA LA BWANA”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 14/06/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 14/06/2026 ni Washarika 853 na Sunday School 250
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Jumapili ijayo tarehe 28/06/2027 kutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae. Hivyo ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi na ibada ya tatu itaanza saa 5.00 asubuhi.
8. NDOA. Hakuna ndoa za washarika
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Hapa Usharikani jumamosi saa moja asubuhi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr na Bibi Ruhago
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Matandiko
- Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Whutson Moshi
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Mama Aida Mwakisu.
- Upanga: Watashiriki ibada ya Maombi na Maombezi hapa Kanisani
10. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
11. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
