DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 NOVEMBA, 2025

SIKU YA BWANA YA MWISHO KABLA YA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

UZIMA WA MILELE UPO KWA AJILI YAKO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 16/11/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 16/11/2025 ni Washarika 688 Sunday School 251

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwashukuru wazazi na walezi kwa kuwa kuwaleta watoto wa kipaimara kwenye mafundisho ya afya jana tarehe 22/11/2025 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 8.00 mchana hapa usharikani. Mungu awabariki sana.

8. Jumanne ijayo tarehe 25/11/2025 saa 11:00 jioni. Kutakuwa na ibada ya kuwapima watoto wa Kipaimara. Wazazi,Walezi na wadhamini mnaombwa kufika kwa wakati.

9. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwatangazia Vijana wote pamoja na washarika kuwa kutakuwa na semina itakayofanyika tarehe 26/11/2025 kwa njia ya mtandao, itakayoanza saa mbili usiku, neno kuu Kijana na uhusiano wake na Mungu. Aidha tarehe 27/11/2025 kutakuwa na maombi ya mfungo yaliyoandaliwa na vijana. Muda wa kukutana ni saa 11 na nusu hapa kanisani Azania kwa ajili ya kuhitimisha kwa pamoja. Na tarehe 05/12/2025 pia Kutakuwa na mkesha wa usiku wa sifa msimu wa tatu hapa Kanisani kuanzia saa tatu usiku mpaka saa kumi na moja alfajiri. Neno kuu Sauti ya shukrani. Washarika wote mnakaribishwa sana.

10. Jumapili ijayo tarehe 30/11/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiande

11. Jumamosi ijayo tarehe 29/11/2025 ni ubarikio kwa watoto wa Kipaimara kwa Kiswahili. Ibada itaanza saa 3.00 asubuhi. na Kingereza itakuwa ni tarehe 06/12/2025. Mavazi kwa wavulana ni Suti nyeusi au suruali nyeusi na shati nyeupe ya mikono mirefu viatu vyeusi. Wasichana gauni jeupe la heshima na viatu vyeupe.

12. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 13/12/2025

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Rayrich Sidon Mosha na Bi. Helena Maria Julita Nyerere

TAREHE 14/12/2025

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Joseph Elihudi Kivulenge na Bi. Jacklina Mchome Joramu

Lakini matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Kenneth Zebedayo

- Upanga: Kwa Mama Magreth Teri

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Christopher Kivulenge

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale.

- Mjini kati: Itafanyika jumamosi hapa kanisani saa 1.00 asubuhi

- Oysterbay, Masaki: Kwa …………………….

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Matandiko

- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Watatangaziana

14. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

15. Zamu za wazee ni fundi la Kwanza

 Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.