Date: 
21-11-2025
Reading: 
Luka 13:29-30

Ijumaa asubuhi tarehe 21.11.2025

Luka 13:29-30

29 Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.

30 Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.

Jiandae kwa hukumu ya mwisho;

Yesu alikuwa akipita mijini na vijijini akifundisha. Mtu mmoja akamuuliza je, wanaookolewa ni wachache? Yesu akamjibu kuwa jitahidini kuingia mlango mwembamba. Yesu alikuwa anawafundisha kuifuata njia yake, maana haikuwa nyepesi, ilihusisha kujikana. Yesu akaendelea kuwaambia ambavyo watakataliwa na Bwana mlangoni akiwaambia "siwajui mimi", huko ndiko kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Ndipo somo letu linakuja, kwamba watatoka watu pande zote za dunia na kuketi chakulani katika Ufalme wa Mungu. Hapa Yesu alitaka wasikilizaji wake wasifikiri ni wao watakaoingia uzimani, bali ni wote waliomwamini na kumcha. Ndiyo maana anamalizia kwa kusema wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho. Tenda yakupasayo ukijiandaa na hukumu ya mwisho. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

Mlutheri