DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 30 NOVEMBA, 2025

SIKU YA BWANA YA 1 KATIKA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

BWANA MWENYE HAKI ANALIJIA KANISA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 23/11/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 23/11/2025 ni Washarika 714 Sunday School ..

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa umoja wa vijana unapenda kuwatangazia Vijana wote pamoja kuwa tarehe 05/12/2025 Kutakuwa na mkesha wa usiku wa sifa msimu wa tatu hapa Kanisani kuanzia saa tatu usiku mpaka saa kumi na moja alfajiri. Neno kuu Sauti ya shukrani. Washarika wote mnakaribishwa sana.

8. Leo tarehe 30/11/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni

9. Uongozi wa Kwaya Kuu unapenda kuwaomba wanakwaya wote wa vikundi vingine kuungana na kwaya Kuu siku ya Jumanne saa 11.00 jioni kwa ajili ya maandalizi ya uimbaji ambao utafanyika ijumaa tarehe 05/12/2025 Kanisa la Anglican St. Alban hapa Posta. Mungu awabariki.

10. Jumamosi ijayo tarehe 06/12/2025 ni ubarikio kwa watoto wa Kipaimara kwa Kingereza. Ibada itaanza saa 3.00 asubuhi. Mavazi kwa wavulana ni Suti nyeusi au suruali nyeusi na shati nyeupe ya mikono mirefu viatu vyeusi. Wasichana gauni jeupe la heshima na viatu vyeupe.

11. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 07/12/2025 katika ibada ya kwanza saa 1.00 asubuhi, familia ya Dr na Mrs Emmanuel Matee watamshukuru Mungu kwa mema mengi aliyowatendea mwaka huu 2025.

Neno: Zaburi 9:1-2, Wimbo: TMW 267 ( Baba yetu aliye Mbinguni)

12. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 13/12/2025

SAA 9.00 ALASIRI

  • Bw. Rayrich Sidon Mosha na Bi. Helena Maria Julita Nyerere

TAREHE 14/12/2025

SAA 8.00 MCHANA

  • Bw. Joseph Elihudi Kivulenge na Bi. Jacklina Mchome Joramu

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Shany Mbogolo

- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mathias Kavugha

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki

- Mjini kati: Itafanyika jumamosi hapa kanisani saa 1.00 asubuhi

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo

14. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tuna kurasa Facebook na Instagram.

15. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili

 Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.

WAZEE WA ZAMU

IBADA YA KWANZA

- Mzee Fred Msemwa - Neno la Waraka

- Mzee Kumbwael Salewi - Matangazo

- Mzee Martha Mkony - Sunday School

- Mzee John Lyanga - Ndoa

IBADA YA PILI

- Mzee Hilda Rwanshane - Neno la Waraka

- Mzee Mcharo Mlaki - Matangazo

- Mzee Samuel Swai - Sunday School

- Mzee Jacqueline Junior Swai - Ndoa

IBADA YA TATU

- Mzee Harold Temu - Neno la Waraka

- Mzee Rehema M. Sanare - Matangazo

- Mzee Rest Barnabas Lasway - Sunday School

- Mzee Rebecca Mwangoka - Ndoa