Date: 
18-10-2023
Reading: 
Marko 11:24-25

Jumatano asubuhi tarehe 18.10.2023

Marko 11:24-25

24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.

Imani isiyo na mashaka;

Yesu anafundisha kusali kwa Imani tukiamini kupokea kutoka kwake. Lakini katika kusali huko, Yesu anafundisha juu ya kusamehe wenzetu ili Baba yetu aliye mbinguni atusamehe. Ipo hoja hapa, kwamba wewe haujamsamehe mwenzako, halafu unataka usamehewe? 

Ujumbe wa Yesu asubuhi hii ni kuomba kwa imani mbele za Mungu wetu. Pia tunakumbushwa kuwa na msamaha kwa wenzetu, ili nasi tupate kusamehewa na Mungu. Tukisameheana tunakuwa na utengemano baina yetu, na Mungu hutusamehe na kutujibu sala sala zetu. Amina.

Jumatano njema.

Heri Buberwa