DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 07 DESEMBA, 2025

SIKU YA BWANA YA 2 KATIKA MAJILIO

 NENO LINALOTUONGOZA NI

CHANGAMKENI MKOMBOZI YU KARIBU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 30/11/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 30/11/2025 ni Washarika 787 Sunday School 221

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo tarehe 07/12/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.

8. Jumapili ijayo tarehe 14/12/2025 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakao hitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

9. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 14/12/2025 familia nne zitamshukuru Mungu.

 Ibada ya Kwanza saa1.00 asubuhi.

- Familia ya Peter James Obama watamshukuru Mungu kwa kusimama nao na kuwapitisha katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao Enna Lutengano Obama, mke na mama wa watoto. Pamoja na mambo mengi aliyowatendea.

Neno: 1Wat0helonike 5:18, Wimbo: 424

- Familia ya Bwana na Bibi Isack Baha wanamshukuru Mungu kwa kuwalinda mwaka mzima na kusherekea mtoto wao Barsiel kutimiza mwaka 1.

Neno Yeremiah 17:7.

 Ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi

- Familia ya Bwana na Bibi Anania Mkota watamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea.

Neno: Wakolosai 3:17, Wimbo: Namshukuru Mungu(Kwaya ya Vijana)

- Familia ya Bwana na Bibi George Mnyitafu Watamtolea Mungu Shukrani Kwa Mema Mengi na baraka nyingi ikiwa ni pamoja na:

Binti yao Dr Isabella G. Mnyitafu kumaliza masomo na kupata shahada ya Udaktari wa Binadamu, Mama Anna Mnyitafu kupona ugonjwa, na Mzee Mnyitafu kufikisha miaka 68 tarehe 13.12. 2025

Neno: Wimbo: Neema ya Ajabu (Kwaya Kuu)

10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 14/12/2025

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Joseph Elihudi Kivulenge na Bi. Jacklina Mchome Joramu

 matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa

- Upanga: Kwa Mama Violet Maro

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mujuni Mutembei

- Kinondoni: Kwa Prof. Geofrey Mmari

- Mjini kati: Itafanyika jumamosi hapa kanisani saa 1.00 asubuhi

- Oysterbay, Masaki: Kwa Mama Elipina Mlaki

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Itemba

- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: …………………………………….

12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

13. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.