Date: 
20-10-2025
Reading: 
Warumi 4:18-25

Jumatatu asubuhi tarehe 20.10.2025

Warumi 4:18-25

18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.

20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;

21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.

22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

23 Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake;

24 bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;

25 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.

Imani Iletayo ushindi;

Mtume Paulo anawaandikia Warumi juu ya Ibrahimu aliyefanywa baba wa mataifa mengi kwa sababu ya Imani yake kwa Mungu. Anasema kwamba Ibrahimu aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa ili apate kuwa baba wa wengi. Pamoja na kuwa na umri mkubwa, Paulo anasema Ibrahimu hakuwa dhaifu wa imani. Ibrahimu aliamini katika Mungu kutimiza ahadi zake, na hakumuacha Bwana.

Paulo anawaita Warumi kumwamini Yesu Kristo mfufuka ili wapate kuhesabiwa haki. Kumbe hatuhesabiwi haki kwa matendo wala vinginevyo, bali kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Asubuhi hii tunakumbushwa kuwa na imani kwa mfano wa Ibrahimu aliyetarajia yasiyoweza kutarajiwa akawa baba wa mataifa mengi. Tumwamini Yesu daima. Amina

Uwe na wiki njema ukiwa na imani.

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com