Date: 
21-03-2022
Reading: 
Yoshua 1:8-9

Hii ni Kwaresma 

Jumatatu asubuhi tarehe 21.03.2022

Yoshua 1:8-9

8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

Tutunze uumbaji;

Baada ya Musa kufa, Mungu alimuita Yoshua na kumpa jukumu la kuongoza wana wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi. Leo asubuhi tunasoma Mungu akimwamuru Yoshua kushika neno na maagizo yake, akiwa hodari na shujaa katika kazi aliyopewa.

Mungu anatualika kumsikiliza kupitia neno lake, tukiamini yuko nasi wakati wote. Kwa neno aliumba dunia na vyote vilivyomo. Kwa kulishika neno hilo hilo, tutunze uumbaji wake, ili dunia iwe mahali salama pa kuishi kwa viumbe vyote.

Uwe na wiki njema, ukitunza uumbaji wa Mungu.