Date: 
18-12-2025
Reading: 
Isaya 56:1-3

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 18.12.2025

Isaya 56:1-3

1 Bwana asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.

2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.

3 Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.

Itengenezeni njia ya Bwana;

Isaya analeta ujumbe wa kulishika neno la Mungu kwa kutenda haki. Anakazia kuwa heri alishikaye neno la Mungu pasipo kufanya uovu. Anatuita kumcha Bwana kwa ibada na matoleo yetu hekaluni mwake, maana nyumba yake ni nyumba ya sala.

Tunaitwa kulishika neno la BWANA tukitenda haki, maana itatuondolea hukumu ya adhabu ya milele. Ibada na matendo mema ni muhimu tunapomngojea Kristo kurudi kwa mara ya pili. Bwana akubariki, ukiwa na siku njema. Amina

Heri Buberwa Nteboya