Date: 
15-10-2025
Reading: 
Yohana 5:10-15

Jumatano asubuhi tarehe 15.10.2025

Yohana 5:10-15

10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.

11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.

12 Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?

13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale.

14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.

15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.

Kristo ametuweka huru;

Ni sikukuu ya Wayahudi huko Yerusalemu, Yesu akiingia hekaluni anakutana na wagonjwa mlangoni waliosuburi maji yachemke, wakiingia humo hupona. Yesu akamkuta mgonjwa aliyekuwa hawezi kwa miaka thelathini na nane, akajieleza kwamba malaika akitibua maji huwa anachelewa kuingia humo. Yesu akamwambia Jitwike godoro lako uondoke. Yule ndugu akajitwika godoro akaondoka akiwa amepona kabisa. Ilikuwa siku ya sabato.

Somo la asubuhi hii linaanzia hapa, Wayahudi hawakuona uhalali wa mgonjwa kuponywa siku ya Sabato. Walihoji uhalali wake kubeba godoro siku ya sabato, maana hawakujua aliyemponya ni nani kwa sababu Yesu alijitenga. Yesu alitokea hekaluni baadaye akamwambia aliyeponywa asitende dhambi tena. Wayahudi hawakuona sahihi mtu kupona siku ya sabato kwa sababu ya kuitunza sabato ya kale. Kumbe Yesu ndiye Bwana wa sabato ambaye ametuweka huru. Anatuita kumwamini siku zote za maisha yetu. Amina

Jumatano njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com