Date: 
14-10-2025
Reading: 
Mathayo 12:1-8

Jumanne asubuhi tarehe 14.10.2025

Mathayo 12:1-8

1 Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.

2 Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.

3 Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe?

4 jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?

5 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?

6 Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.

7 Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.

8 Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

Kristo ametuweka huru;

Somo la leo asubuhi ni sawa na lile la jana asubuhi, wanafunzi wanavunja masuke mashambani na kuyala na Mafarisayo wakashangaa na kumuuliza Yesu ni kwa nini walifanya vile? Hii ilikuwa siyo halali siku ya sabato! Yesu anawakumbusha jinsi Daudi alivyohisi njaa akala mikate hekaluni na wenzake ambayo ilitakiwa kuliwa na makuhani peke yao. Katika Injili ya Mathayo, Yesu anaongezea kwamba makuhani hekaluni waliinajisi sabato wasipate hatia, yaani walitenda yawapasayo na sabato ikabaki palepale.

Yesu anaongezea kwamba yupo aliye mkuu kuliko hekalu, hapa alikuwa anajiongelea yeye mwenyewe. Anaendelea kusema anataka rehema na wala siyo sadaka. Anahitimisha kwamba yeye ndiye Bwana wa sabato. Yesu aliwafundisha kumtazama yeye aliye Bwana wa sabato. Nasi tumtazame Yesu aliyetuweka huru. Amina

Jumanne njema

Heri Buberwa Nteboya 

Mlutheri 

0784 968650