Date:
22-08-2025
Reading:
Muhubiri 9:17-18
Ijumaa asubuhi tarehe 22.08.2025
Mhubiri 9:17-18
17 Maneno ya wenye hekima yanenwayo taratibu husikiwa, Zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya wapumbavu.
18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.
Tuenende kwa hekima ya Mungu;
Katika sehemu hii tunasoma juu ya nguvu ya hekima ya Mungu. Ukianzia nyuma kidogo unaona Mfalme Suleimani akitoa mfano wa jinsi hekima ya mtu mmoja tena maskini ilivyouokoa mji uliokuwa ushambuliwe na kuangamizwa na mfalme aliyeujia kwa nia ovu. Habari hiyo inapatikana kabla ya somo kama unavyoweza kusoma;
Mhubiri 9:14-16
14 Palikuwa na mji mdogo, na watu ndani yake walikuwa wachache; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga. 15 Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini. 16 Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.Baada ya mfano huo ndipo somo la asubuhi hii linafuatia kwa kuonesha nguvu ya hekima ya Mungu kwa waaminio. Suleimani anasema kwamba hekima inayo nguvu kuliko mlio wa atawalaye katikati ya wapumbavu! Hitimisho lake ni kwamba hekima ndiyo bora kupita silaha za vita. Kumbe asubuhi hii tuhitimishe kwamba hekima ya Mungu ndiyo ifaayo kwetu tuaminio. Basi tuombe hekima ya Mungu isipungue kwetu, ili tuwaze, tuseme na kutenda kwa utukufu wa Mungu. Amina
Ijumaa njema
Heri Buberwa Nteboya
Mlutheri
0784 968650