MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 29 SEPTEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA 8 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

TUWAJALI WATOTO WETU KATIKA BWANA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 22/09/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei yaTsh. 40,000/=. 

7. Jumatano ijayo tarehe 02/10/2024 kutakuwa na kikao cha Baraza la Wazee. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati.

 ​​​​​​8. Jumapili ijayo tarehe 06/10/2024 itakuwa ni sikukuu ya mavuno. Washarika tujiandae na kuiombea siku hiyo. Sare itakuwa ni kitenge chetu cha Kiharaka. Aidha siku hiyo tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

9. Umoja wa Vijana Azania Front umeandaa ibada ya mkesha maalum unaoitwa "Night of Praise (Season II)" uliobeba kichwa cha mwaka "Sing His Greatness," Kutoka katika Zaburi 145:3. Mkesha huu utafanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front ijumaa ijayo tarehe 4 Oktoba 2024, kuanzia saa mbili usiku hadi alfajiri. Vikundi mbalimbali vya uimbaji vitashiriki, pamoja na paneli ya majadiliano kuhusu afya ya akili (Mental Health), na matukio mengine ya kipekee.Tshirt maalumu kwa hiyo siku zinapatikana nnje kwa Tsh 20,000/= mikono mifupi na Tsh 25,000/= mikono mirefu..

10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

Hakuna ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mruma
  • Mjini kati: Kwa Mama Victoria Mwansasu
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa ………… .
  • Kinondoni: Kwa Profesa na Bibi Kulaba
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bi. Elyfrida Njowoka Edwin
  • Kwa Bi. Elyfrida Njowoka Edwin
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Profesa William Matuja
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: ……………………………………….. 
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Bwana Abdiel Mengi.

13. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza watashirikiana na watoto.  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu,

Bwana ayabariki.