MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 05 MEI, 2024

SIKU YA BWANA YA 5 BAADA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

OMBENI NANYI MTAPATA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 28/04/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Leo tarehe 05/05/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.

6. Alhamisi ijayo tarehe 09/05/2024 saa 11.00 jioni tutakuwa na ibada ya kukumbuka kupaa kwa Bwana Yesu kristo. Kwaya zote zitahudumu. Zamu za wazee itakuwa ni kundi la pili

7. Jumapili ijayo tarehe 12/05/2024 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Washarika wanaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

8. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unaomba kuwakumbusha Washarika waliochukua bahasha za kusaidia kulipa Ada za Watoto Yatima wa Kituo cha Watoto Yatima cha Don Bosco kukamilisha ahadi zao na kurudisha bahasha kwa viongozi wa Umoja wa wanawake au ofisini kwa Parish Worker. Asanteni sana, Mungu awabariki.

9. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 18/05/2024 ITAKAYOFUNGWA SAA 9.00 ALASIRI KATI YA

  • Bw. Emmanuel Hezron Mkonyi na Bi. Dianna Hardson Massawe

Tangazo hili limebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Watatangaziana
  • Mjini kati: Kwa Mama Omega Mongi.
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Korosso.
  • Kinondoni: Kwa ……………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana Allen David  
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Watashiriki ibada ya kupaa hapa Kanisani.
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa …………………..
  • Oysterbay, Masaki: Kwa …………………….

11. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.