MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 10 JULAI, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
KIJANA NA UCHUMI KATIKA ZAMA ZA UTANDAWAZI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 03/07/2022
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
5. SEMINA:
Tunawakaribisha wote kushiriki katika kujifunza Neno la Mungu, katika Semina ya siku 5 itakayoanza kesho Jumatatu tarehe 11 Julai 2022, saa 11:00 jioni hapa Kanisa Kuu Azania Front. Mwl Musa Musa atafundisha. Ni chakula kilichotayarishwa kwa ajili yetu. Kwaya zetu zitahudumu.
6. Leo tarehe 10/07/2022 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika Karibuni.
7. SHUKRANI
Jumapili ijayo tarehe 17/07/2022 katika ibada ya Tatu saa 4.30 asubuhi familia ya Bwana na Bibi Allen na Anna Kaduri watamshukuru Mungu kwa Mzee Allen kutimiza miaka 85 ya kuzaliwa, Miaka 55 ya Ndoa yao pamoja na mambo mema mengi aliyowatendea kwenye familia yao.
Neno: Zaburi 23:4-6, Wimbo: TMW 295
8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
Kwa mara ya Pili tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 23/07/2022
SAA 10:00 JIONI
Bw. Raymond Mathew Munisi na Bi. Doris Elishilia Sindila
Kwa mara ya Tatu tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 16/07/2022
SAA 10:00 JIONI
Bw. Victor Remmy Machange na Bi. Jesca Edward Mollel
Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.
9. NYUMBA KWA NYUMBA
Masaki na Oyserbay: Kwa Mzee Elipina Mlaki
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Raymond Sangiwa
- Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
- Kinondoni: Kwa Prof na Bibi S. Kulaba
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Zimba
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Watatangaziana
10. Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili watashirikiana na Vijana.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki