MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 08 JULAI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI 'UPENDO WA MUNGU NA UTAWALE'

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Wageni waliotufikia na cheti ni Simon Tweve – toka kanisala Anglikana - Kongowe

3. Tunamshukuru Mungu kwa jinsi anavyojidhihirisha kila tunapokutana kwa masomo, maombi na maombezi. Hivyo kuanzia jumatatu tarehe 09/07/2018  hadi ijumaa tarehe 13/07/2018 tutaendelea na kipindi cha Morning Glory kikiongozwa na Mwl. Mgisa Mtebe.  Aidha siku ya alhamisi tarehe 12/07/2018 kuanzia saa 11.30 jioni tutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi.  Washarika wote mnakaribishwa. 

4. Leo ni sikukuu ya Umoja wa Vijana hivyo ibada zote zitaongozwa na vijana.

5. Jumamosi ijayo tarehe 14/-7/2018 ni siku ya tamasha la uimbaji wa kwaya ya Wanawake.  Tamasha hili litafanyika Usharika wa Kitunda Relini.  Hivyo wiki hii kutakuwa na mazoezi siku ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.  Wanawake wote wanaombwa kushirikiana pamoja katika kumsifu Mungu.

6. Jumapili ijayo tarehe 15/07/2018 katika ibada ya pili  familia ya Marehemu Theogoni Amrini pamoja na kwaya ya Vijana watamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kuwafanikisha kumaliza msiba salama.

7. Neno: Zaburi 103:1-22, Wimbo: Kwaya ya Vijana

 

   8.  NDOA.

  NDOA ZA WASHARIKA

  KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 21/07/2018 SAA 08.00 MCHANA

Bw. Mika Mathayo Ndosa         na     Bi Marystela Kondo Benedict

SAA 09.00 ALASIRI

Bw. Amani Goodluck Kamnde     na     Bi Anna Cecilia Katarina Westman

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu

 

9. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula

      Mjini kati:  Kwa Mama Omega Mongi

Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo

Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi David Korosso

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili watashirikiana na Vijana.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.