MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 05 FEBRUARI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI SIKU YA KUNG’AA KWA YESU

  1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
  1. Wageni: wageni waliotufikia na cheti ni
  • Augustine N. Kyando toka Usharika wa Mbeya mjini KKKT, Dayosisi ya Konde – anahamia hapa Azania Front.
  1. Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya uongozi wa Usharika inapenda kuwatangazia washarika wote kuwa kutakuwa na Semina ya Neno la Mungu ya siku 8, kuanzia leo jumapili tarehe 05.02.2017 kuanzia saa 9.00 alasiri mpaka tarehe 12.02.2017 hapa Usharikani. Siku za katikati ya juma semina itaanza saa 11.30 jioni, jumamosi itaanza saa 10.00 jioni.  Kichwa cha somo ni NAMNA YA KUONDOA MFUMO WA SHETANI NDANI YAKO ILI UFANIKIWE KIROHO NA KIMWILI. Yn. 3:8b, Mnenaji atakuwa ni Mwinjilisti Baraka Mbise toka KKKT Ubungo.  Semina hii imeandaliwa  kwa ajili ya washarika wa Kanisa Kuu la Azania front. Watakaohudumu ni Wazee wa Baraza Azania Front na kwaya zote za hapa usharikani. Washarika wote mnaombwa kuhudhuria. 
  1. Leo tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
  1. Jumapili ijayo tarehe 12/02/2017 kutakuwa na ubatizo wa watoto na kurudi kundini.  Washarika watakaohitaji huduma hii wafike ofisi ya Mchungaji.
  1. Jumapili ijayo tarehe 12.02.2017 katika ibada ya pili saa 3.30 asubuhi, familia ya Bwana na Bibi Isaac Mfalila watamshukuru Mungu kwa kutimiza miaka mitatu ya ndoa, kupata mtoto wa pili,afya na maendeleo ya familia pamoja na mambo mengi aliyowatendea.

Neno: Wafilipi 4:6-7, Wimbo: Na. 168

  1. Usharika umepata mwaliko wa kutembelea Usharika rafiki wa Messiah, ulioko Marguette Michigan Marekani kati ya tarehe 5-19 mwezi wa Oktoba mwaka huu.  Ujumbe utakuwa na watu 10, nusu wanawake, nusu wanaume.  Wenyeji watahusika na malazi, chakula na usafiri. Washarika watagharamia usafiri wao wenyewe kiasi cha USD 2,000/= kwa tiketi ya ndege kwenda na kurudi, pamoja na Visa, USD 200 hadi 500 kwa matumizi binafsi.  Watakaopenda kujiunga kwenye ziara hii, wajiandikishe ofisini kwa katibu wa Chaplain mapema.  Taarifa muafaka zitaendelea kutolewa jinsi mipango inavyosonga mbele.
  1. Usharika una mpango wa kuandaa kijarida kwa ajili ya kuwajuza washarika kuhusu shughuli, mipango, matukio, na mengineyo yanayohusu Usharika na mitaa inayotunzwa na Usharika.  Kijarida hicho kitakuwa kinatolewa kila baada ya miezi 3.  Tunaomba vijana 2 wa kujitolea wenye taaluma ya habari au ujuzi husika, kwa ajili ya kukusanya habari na kuandaa kijarida hicho. Wawasiliane na Mzee Theophilus Mlaki, Mzee Cuthbert Swai, au ofisi ya Usharika mapema iwezekanavyo.
  1. Tunapenda kuwatangazia kuwa wavuti (website) ya Kanisa Kuu Azania Front – www.azaniafront.org imeboreshwa na inafanya kazi vizuri na katika mwonekano mpya.  Jitahidi kila siku ufungue wavuti (website) hiyo ili upate neno la kila siku na habari nyingine za Usharika.  Inapatikana kupitia Compyuta, pad na hata simu zetu.
  1. NDOA:

Kwa mara kwanza tunatangaza ndoa za tarehe 25/02/2017

Bw. Efraim Simon Mwaipungu                na     Bi. Doris Jamesy Ambangile

Kwa mara tatu  tunatangaza ndoa za tarehe 11/02/2017

Ndoa hii ifuatayo itafungwa usharika wa KKKT Msasani

Bw. Maleke Hans Mringo               na     Bi. Daines Joyce Zimba

 Matangazo mengine yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu

  1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
  • Upanga: Watangaziana
  • Kinondoni:  Kwa Bwana  na Bibi Danford Mariki
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa dada Elifrida Njowoka
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watangaziana
  • Oysterbay/Masaki: Watangaziana
  • Tabata: Watangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Zebedayo
  • Mjini kati: Watangaziana
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:  Kwa Bwana na Bibi Moshi