MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 12 MACHI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UKATILI NI UOVU

  1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
  1. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti.
  1. Leo hatutakuwa na ibada ya maombi hapa Usharikani badala yake tutaungana na wenzetu kwenye semina itakayoongozwa na Mwalimu Christopher Mwakasege inayofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers (Kawe) kuanzia saa 8.00. Aidha siku ya alhamisi  tarehe 16.03.2017 saa 11.30 jioni kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi hapa usharikani ambacho kitaongozwa na mtumishi Baraka Mbise toka KKKT Ubungo. Wote mnakaribishwa.
  1. Umoja wa vijana Azania Front unapenda kuwataarifu washarika na vijana wote watakaopenda kuhubiri kwa njia ya igizo la mateso ya Yesu wakutane hapo nje kwenye jukwaa baada ya ibada. Mnakaribishwa sana.
  1. Jumatano ijayo tarehe 15/03/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada kama kawaida ya Kwaresma.  Zamu za wazee itakuwa ni kundi la kwanza. Aidha  Ratiba nzima ya ibada siku za jumatano imebandikwa kwenye ubao wa matangazo mlango mkuu kwenye bahasha za Ahadi na nje Karibu na duka letu la vitabu.
  1. Kwaya ya Umoja itakuwa na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Kantate siku ya Jumanne ijayo tarehe 14/03/2017 saa 11.00 jioni.  Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati.
  1. Familia ya Bwana na Bibi Desmond Malyi wamepata zawadi ya mtoto wa kiume tarehe 05/03/2017 katika hospitali ya Taifa Muhimbili. Baba, mama na mtoto wanaendelea vizuri.
  1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

 

  • Upanga: Watangaziana
  • Kinondoni:  Kwa Dada Niwaeli Mziray
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watangaziana
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watangaziana
  • Oysterbay/Masaki: watashiriki ibada hapa usharikani
  • Tabata: Watangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  • Mjini kati: Kwa Mama Twilumba Talawa
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mpuya

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.