Date: 
23-01-2017
Reading: 
Mark 7:24-30 New International Version (NIV)

MONDAY 23RD JNAUARY 2017 MORNING                      

Mark 7:24-30 New International Version (NIV)

Jesus Honors a Syrophoenician Woman’s Faith

24 Jesus left that place and went to the vicinity of Tyre.[a] He entered a house and did not want anyone to know it; yet he could not keep his presence secret. 25 In fact, as soon as she heard about him, a woman whose little daughter was possessed by an impure spirit came and fell at his feet. 26 The woman was a Greek, born in Syrian Phoenicia. She begged Jesus to drive the demon out of her daughter.

27 “First let the children eat all they want,” he told her, “for it is not right to take the children’s bread and toss it to the dogs.”

28 “Lord,” she replied, “even the dogs under the table eat the children’s crumbs.”

29 Then he told her, “For such a reply, you may go; the demon has left your daughter.”

30 She went home and found her child lying on the bed, and the demon gone.

Footnotes:

  1. Mark 7:24 Many early manuscripts Tyre and Sidon

Jesus was born as a Jew and initially His ministry was to Jews. In His reply to the Greek woman Jesus at first appears to show discrimination. However He was seeking to draw out her faith. Jesus praised her faith and He agreed to heal her daughter.

Jesus did not come to the Jews only. Jesus came for all people. He loves you what every your background and He wants you to trust in Him.

JUMATATU TAREHE 23 JANUARI 2017, ASUBUHI                          

MARKO 7:24-30

24 Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika. 
25 Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake.
 26 Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake. 
27 Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. 
28 Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto. 
29 Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako. 
30 Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka. 
 

Yesu alikuja duniani kama Myahudi. Huduma yake mwanzoni ilionekana ni kwa Wayahudi tu. Jibu lake mwanzoni kwa Yule Mwanamke Myunani ilionekana kuwa ya kibaguzi. Lakini lengo la Yesu lilikuwa ni kuthibitisha imani yake. Yesu alisifu imani ya Yule mama na alikubali kumponya binti yake.

Yesu amekuja duniani si kwa wayahudi tu, bali kwa kila mtu. Yesu anakupenda hajali umetoka wapi. Yesu anataka umwamini na umtegemea katika maisha yako.