Date: 
31-03-2017
Reading: 
Exodus 16:11-15 (NIV)

FRIDAY 31ST MARCH 2017 MORNING                                    

Exodus 16:11-15 New International Version (NIV)

11 The Lord said to Moses, 12 “I have heard the grumbling of the Israelites. Tell them, ‘At twilight you will eat meat, and in the morning you will be filled with bread. Then you will know that I am the Lord your God.’”

13 That evening quail came and covered the camp, and in the morning there was a layer of dew around the camp. 14 When the dew was gone, thin flakes like frost on the ground appeared on the desert floor. 15 When the Israelites saw it, they said to each other, “What is it?” For they did not know what it was.

Moses said to them, “It is the bread the Lord has given you to eat.

God provided food for the Israelites in the dessert. In the Lord’s Prayer we are encouraged to ask God to provide our Daily Bread. Jesus said that we also need spiritual food daily which we find when we read God’s Word. Also Jesus Himself is the Bread of Life. Jesus sustains our lives and He is the one who gives us Eternal Life.

IJUMAA TAREHE 31 MACHI 2017 ASUBUHI                         

KUTOKA 16:11-15

11 Bwana akasema na Musa, akinena, 
12 Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Israeli; haya sema nao, ukinena, Wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 
13 Ikawa wakati wa jioni, kware wakakaribia, wakakifunikiza kituo; na wakati wa asubuhi umande ulikuwa juu ya nchi pande zote za kituo. 
14 Na ulipoinuka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama sakitu juu ya nchi. 
15 Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao Bwana amewapa ninyi, mle. 
 

Mungu alilisha Waisraeli jangwani. Yesu katika Sala ya Bwana anatufundisha tumwombe Mungu atupe chakula chetu cha kila siku. Pia Yesu alisema kwamba hatuishi kwa mkate tu bali kwa Neno la Mungu. Yesu mwenyewe alisema yeye ni Chakula cha Uzima. Tumshukuru Mungu anatupa chakula cha kimwili lakini tukumbuke pia umuhimu wa kusoma Neno la Mungu kila siku na kumtegemee Yesu kama Bwana na Mwokozi wetu. Yesu anatupa Uzima wa Milele.