Date: 
28-03-2017
Reading: 
2 Corinthians 7:13-16 (NIV)

TUESDAY 28TH MARCH 2017 MORNING                                

2 Corinthians 7:13-16  New International Version (NIV)

13 By all this we are encouraged.

In addition to our own encouragement, we were especially delighted to see how happy Titus was, because his spirit has been refreshed by all of you. 14 I had boasted to him about you, and you have not embarrassed me. But just as everything we said to you was true, so our boasting about you to Titus has proved to be true as well. 15 And his affection for you is all the greater when he remembers that you were all obedient, receiving him with fear and trembling. 16 I am glad I can have complete confidence in you.

These verses written in a letter from the Apostle Paul to the church in Corinth show us the importance of Christian fellowship.  Paul had sent Titus to visit the Church at Corinth to see their progress and to advise and encourage them.  We need to meet together to encourage and advise and warn and correct one another so that we can all be strengthened in our faith and bear spiritual fruit.

JUMANNE TAREHE 28 MACHI 2017 ASUBUHI                        

2 KORINTHO 7:13-16

13 Kwa hiyo tulifarijiwa. Tena katika kufarijiwa kwetu tulifurahi sana kupita kiasi kwa sababu ya furaha ya Tito; maana roho yake imeburudishwa na ninyi nyote. 
14 Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli. 
15 Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi, akumbukapo kutii kwenu ninyi nyote, jinsi mlivyomkaribisha kwa hofu na kutetemeka. 
16 Nafurahi, kwa sababu katika kila neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu.

Mtume Paulo  alimtuma Tito kutembelea Wakristo kule Korintho. Alitaka kujua hali yao na kuwatia moyo. Tunaona jinsi wote walivyofarijiana. Hapa tunakumbushwa umuhimu wa wakristo kukutana pamoja mara kwa mara kutiana moyo, kufarijiana na pia ikibidi kuonyana na kusahihishana. Lengo ni sote tukue kiroho na tuzae matunda ya kiroho.