Date: 
02-04-2017
Reading: 
Psalm 119:121-128, Luke 23:8-12, 1 John 3:2-6 (NIV)

SUNDAY 2ND APRIL 2017

THEME: JESUS IS  THE PEACEMAKER

Psalm 119:121-128, Luke 23:8-12, 1 John 3:2-6 (NIV)

 

Psalm 119:121-128   

ע Ayin

121 I have done what is righteous and just;
    do not leave me to my oppressors.
122 Ensure your servant’s well-being;
    do not let the arrogant oppress me.
123 My eyes fail, looking for your salvation,
    looking for your righteous promise.
124 Deal with your servant according to your love
    and teach me your decrees.
125 I am your servant; give me discernment
    that I may understand your statutes.
126 It is time for you to act, Lord;
    your law is being broken.
127 Because I love your commands
    more than gold, more than pure gold,
128 and because I consider all your precepts right,
    I hate every wrong path.

 

Luke 23:8-12   

When Herod saw Jesus, he was greatly pleased, because for a long time he had been wanting to see him. From what he had heard about him, he hoped to see him perform a sign of some sort. He plied him with many questions, but Jesus gave him no answer. 10 The chief priests and the teachers of the law were standing there, vehemently accusing him. 11 Then Herod and his soldiers ridiculed and mocked him. Dressing him in an elegant robe, they sent him back to Pilate. 12 That day Herod and Pilate became friends—before this they had been enemies.

 

1 John 3:2-6   

Dear friends, now we are children of God, and what we will be has not yet been made known. But we know that when Christ appears,[a] we shall be like him, for we shall see him as he is. All who have this hope in him purify themselves, just as he is pure.

Everyone who sins breaks the law; in fact, sin is lawlessness. But you know that he appeared so that he might take away our sins. And in him is no sin. No one who lives in him keeps on sinning. No one who continues to sin has either seen him or known him.

Footnotes:

  1. 1 John 3:2 Or when it is made known

Jesus is the peacemaker.  He died for us so that our sins can be forgiven and we can be reconciled to God.  We can not make ourselves acceptable to God by our own efforts but Jesus paid the price. Let us trust in Him.

JUMAPILI  TAREHE 2 APRILI 2017

NENO KUU: YESU NI MPATANISHI

Zaburi 119:121-128

121 Nimefanya hukumu na haki, Usiniache mikononi mwao wanaonionea. 
122 Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema, Wenye kiburi wasinionee. 
123 Macho yangu yamefifia kwa kuutamani wokovu wako, Na ahadi ya haki yako. 
124 Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe. 
125 Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe, Nipate kuzijua shuhuda zako. 
126 Wakati umewadia Bwana atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako. 
127 Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi. 
128 Maana nayaona mausia yako yote kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia. 
129 Shuhuda zako

 

Luka 23:8-12

8 Na Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona tangu siku nyingi, maana amesikia habari zake, akataraji kuona ishara iliyofanywa na yeye. 
9 Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lo lote. 
10 Wakuu wa makuhani na waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana. 
11 Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato. 
12 Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao. 
 

1 Yohana 3:2-6

2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 
3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. 
4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 
5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 
6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 
 

Yesu ni Mpatanishi. Yesu ni njia pekee kufikia kwa Mungu Baba. Binadamu tu wenye dhambi na hatustahili kumsogelea Mungu Mtakatifu. Lakini Yesu alilipa deni kwa kutufia mnsalabani. Basi tumtegemea Yesu na tutubu dhambi zetu na kupokea wokovu kwa neema.