Date:
22-01-2026
Reading:
1 Samweli 1:26-28
Hii ni Epifania
Alhamisi asubuhi 22.01.2026
1 Samweli 1:26-28
26 Akasema, Ee bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba Bwana.
27 Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba;
28 kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko.
Nyumba zetu hubarikiwa na Mungu;
Elkana alikuwa na wake wawili, Hana na Penina. Hana hakuwa na mtoto, Penina alikuwa na watoto. Penina alimcheka sana Hana na kumdhihaki, jambo ambalo lilimuumiza sana Hana. Hana alikaa hekaluni akiomba mtoto toka kwa Mungu, ahadi yake kwa Mungu ilikuwa kumtoa mtoto huyo kumtumikia Mungu daima.
Somo la asubuhi hii ni shukrani ya Hana kwa Mungu baada ya kupata mtoto ambaye ni Samweli. Hana anajitambulisha kwa Bwana kwamba ndiye yule mwanamke aliyeomba mtoto. Anarudia ahadi yake ya mtoto huyo kumtumikia Mungu daima. Kwa kumwomba Mungu Hana alipata mtoto. Nasi tukimtegemea Bwana anabariki nyumba zetu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
